Waziri Mkuu aliejiuzuru na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Arusha,Mzee Jackson Kaaya nyumbani kwake Poli Meru wakati alipofika kumuona na kumsabahi.Pembeni ni mkewe Bibi Jacobert Kaaya.
Mzee Kaaya mwenye umri wa miaka 94 alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TANU Mkoa wa Arusha hadi alipostaafu mwaka 1984.
Mh. Lowassa alikuwa Katibu wa Chama wa mkoa enzi za uenyekiti wa Mzee Kaaya na ndiye aliyemfudisha uongozi wa kisiasa.
Katika maongezi yao Mzee Kaaya amesema anasikitishwa na viongozi wa kizazi hiki kwa kuongoza kwa kulalamika badala ya kuchapa kazi.
0 comments:
Post a Comment