Mkazi wa Kyela mkoani Mbeya, Mboka Mwakikagile (20) akiwa na mtoto wake Godluck Mwangosi katika Hospitali ya Rufaa Meta ya jijini Mbeya baada ya polisi kumkamata mtu anayedaiwa kumwiba mtoto huyo. Picha ya Maktaba
Dar es Salaam. Kwa muda mrefu kumekuwapo na taarifa za watoto kupotea katika mazingira tofauti, huku baadhi yao wakipatikana na kuunganishwa tena na wazazi wao, lakini wengine hawajaonekana hadi leo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mikoa mbalimbali nchini kubaini sababu za watoto hao kupotea, umebaini kuwa baadhi ya watoto huondoka nyumbani baada ya kutokea ugomvi kati ya wazazi au walezi wao.
Sababu nyingine ni kuibuka kwa biashara ya watoto wanaouzwa kwa watu ambao hawana watoto, nchini na nje ya nchi na imani za kishirikina zinazochochewa na waganga wa jadi.
Taarifa kutoka polisi zinasema kuwa baadhi ya watoto walioripotiwa kwenye vituo vya polisi kupotea au kuibwa, walibainika kuchukuliwa na mmoja wa wazazi wa mtoto kutokana na migogoro kwenye familia.SOMA ZAIDI>>>>>>>>>
0 comments:
Post a Comment