Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe
(Kulia) akila kiapo cha utii na utumishi mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete
(Kushoto).
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe
akisaini hati ya kiapo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto) akimkabidhi vitendea
kazi Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi)
mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya
kumuapisha.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Aliyeinama) akiwapa zawadi
watoto wa Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul
Sangawe (Kulia) mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango atakayesimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa
katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe
(Wapili kulia) mara baada ya kuapishwa.
Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akizungumza na wanahabari mara baada ya
kuapishwa na kukabidhiwa jukumu la kusimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi.
Shangwe na vigelegele!
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimpokea
kwa shangwe na vigelegele Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa
jukumu la Naibu Katibu Mtendaji katika Ofisi hiyo ambaye atasimamia masuala ya
Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.Picha zote na Saidi
Mkabakuli-Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
---
Na Saidi Mkabakuli
Serikali imeweka wazi mkakati wa kuainisha fursa za
kipaumbele zitakazoiwezesha kuivusha nchi kikanda na kimataifa kwa kusimamia na
kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama inavyobainishwa na Mpango wa
Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Miaka Mitano (FYDP I) unaosimamiwa na Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango.
Mkakati huo umewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji mpya
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi Bw. Paul Sangawe mara baada ya kula kiapo cha kuitumika
nafasi hiyo.
Bw. Sangawe amesema kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma pamoja na kufaidika na misaada
kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa.
“Kwa mujibu wa Mpango Wa Maendeleo
Wa Taifa Mwaka 2012/13 thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilikuwa dola za
Kimarekani 6,796.3 milioni mwaka 2011, ikilinganishwa na dola 5,805.0 milioni
mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 17.1. hivyo mkakati wetu ni kuongeza
hali hii,” alisema Bw. Sangawe.
Kwa mujibu wa Mpango huo thamani ya
bidhaa za kukuza mitaji zilizoagizwa toka nje iliongezeka hadi dola za
Kimarekani 3,560.5 milioni kutoka dola 2,715.2 milioni mwaka 2010, sawa na
ongezeko la asilimia 31.1. Ongezeko hili lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa
uagizaji wa mitambo hasa ile ya viwandani.
Aidha, thamani ya uagizaji wa
bidhaa za kati iliongezeka hadi dola za Kimarekani 4,139.0 milioni mwaka 2011,
kutoka dola 2,741.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 51.0.
Uagizaji wa mafuta kwa wingi ulitokana na matatizo yaliyojitokeza ya
kutozalishwa kwa kiasi kinachohitajika cha umeme unaotokana na maji, hivyo
kupelekea mitambo mingi ya mashine kuendeshwa kwa kutumia umeme unaozalishwa na
mafuta.
Vilevile, thamani ya mafuta
yaliyoagizwa katika mwaka 2011 ilikuwa dola milioni 3,228.7 ikilinganishwa na
dola milioni 2,024.2 mwaka 2010. Uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida
uliongezeka hadi dola 2,128.0 milioni kutoka dola 1,709.2 milioni mwaka 2010,
sawa na ongezeko la asilimia 24.5.
Bw. Sangawe ameongeza kuwa Serikali inajikita katika
kutambua masoko kwa bidhaa za Tanzania na vyanzo vipya vya uwekezaji katika
uchumi wa Dunia na Kikanda ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia kufanikisha
utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ili kuwezesha nchi kuchanmkia fursa za
masoko ya kimataifa ikiwemo AGOA na nchi za jumuiya za Ulaya.
“Kipaumbele itakuwa ni kutumia rasilimali chache
kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele na ya
matokeo makubwa,” aliongeza Bw. Sangawe.
Serikali imeaandaa Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa
kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania
kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
0 comments:
Post a Comment