Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick
Werema
--
Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na kulinywa mwenyewe’, baada ya
jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake
visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na
kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu
mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na
kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi
Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.
Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa
Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na
majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa
ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka
2014/15.Kwa habari zaidi Bofya
na Endelea......
0 comments:
Post a Comment