Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akisalimiana na Mbunge wa Urambo Ndugu John Samuel Sitta wakati wa mapokezi
katika kijiji cha Izimbili wilaya ya Urambo mkoani Tabora,Katibu Mkuu atakuwa
kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Urambo ambapo atakagua utekelezaji
wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 na uhai wa Chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akisalimiana na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Tabora Magreth Sitta wakati wa
mapokezi katika kijiji cha Izimbili wilaya ya Urambo mkoani Tabora,Katibu Mkuu
wa CCMatakuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Urambo ambapo
atakagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 na uhai wa
Chama
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Izimbili wilayani Urambo mkoa wa
Tabora.
Umati wa wananchi wa kijiji cha Izengabatogilwe ukiwa
nje ya jengo la Zahanati,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alitembelea
zahanati hiyo na kukagua maendeleo ya zahanati hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Izengabatogilwe wakati wa ukaguzi wa
mradi wa zahanati ya kijiji hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua
vyumba vya zahanati ya kijiji cha Izengabatogilwe
Zahanati ya kijiji cha
Izengabatogilwe
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Uyumbu akishirikiana na Mbunge wa
Urambo Ndugu John Samuel Sitta.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa
kwenye picha ya pamoja na kikundi cha ulinzi shirikishi cha kijiji cha
Izengabatogilwe pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na mbunge
wa Urambo Ndugu John Samuel Sitta.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua
shamba la mahindi kwenye Mradi wa Shamba Darasa kituo cha kilimo cha Matone
katika kijiji cha Kapilole ,Urambo.
Shamba la mahindi katika kituo cha Kilimo cha matone
katika kijiji cha Kapilole,Urambo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa
kwenye picha ya pamoja na wakulima kituo cha Kilimo cha Matone,wengine pichani
ni Mbunge wa Urambo Ndugu John Samuel Sitta na Mbunge wa Viti Maalum Magreth
Sitta.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Mabatini pamoja na Mbunge wa Urambo Ndugu John
Samuel Sitta na wana CCM wengine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia
vitanda vya wodi ya Mama Ngojea kwenye hospitali ya wilaya ya Urambo,ambapo wodi
hiyo itasaidia sana wakina mama kujifungua salama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini
vitabu vya wageni kabla ya kuanza kwa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya
ya Urambo,wengine pichani ni Mbunge wa Urambo John Samuel Sitta na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya
Urambo wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
0 comments:
Post a Comment