(Picha
zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi
wetu
Ngorongoro
Crater ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia ukiwamo Mlima Kilimanjaro. Ni
mwendo wa sana Tumbili na Nyani aina mbalimbali. Na usipokuwa mwangalifu na
kuacha milango na madirisha wazi Soda, Biskuti na Ndizi mbivu ulizochukua kwa
kujikimu na njaa ya siku nzima ukiwa mbugani, utakuta hakuna hata nyaraka.
Kama watazisoma au hapana hilo si jukumu lako ila utakuwa umepoteza nyaraka
muhimu.
Ngorongoro
Crater ni mbuga za wanyama mfano wa bakuli kubwa lililoundwa miaka 25 elfu
iliyopita baada ya milima miwili Makaroti na Satiman kulipuka na kutoa tope
lenye moto. Tope hili ndilo lilikuwa na tabaka tatu za udongo na kuumba bonde
lililofanana na bakuli kubwa ambalo wenyeji wa kabila la Kimasai walilipa jina
la Ngorongoro Kaldera.
Kijiji cha
Malanja ni cha pekee katika bonde la Ngorongoro katikati ya Milima ya Makaroti
ambao ni mkubwa na Satiman ambao ni mdogo. Wenyeji wa kijiji hicho huendesha
Maisha yao kama kawaida ya kufuga mifugo yao ndani ya mbuga wakichanganyika na
wanyama pori.
Katika bonde
hilo kuna mto mmoja ambao unatoka Olmot Crater, Ziwa Magadi ambalo wakati wa
kiangazi hukauka na kutoa vumbi aina ya majivu ambayo wenyeji wa Kimasai hutumia
kuwalisha Ng’ombe kama dawa ya kudhibiti magonjwa.
Huwezi
kuzungumzia hifadhi ya Ngorongoro Crater bila kuwataja wanyama wakubwa
wajulikanao kama “Big Five”, ambao ni Faru, Tembo, Chui, Nyati na Simba. Lakini
kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa utalii, Kwa sasa kuna Big Six akiwemo
Mmasai kwa kile kinachoitwa kuwa karibu na mbuga hiyo na kuishi na wanyama bila
kudhuriana.
Twiga pamoja
na kwamba anatajwa kuwa miongoni mwa wanyama wanaotajwa kuwemo katika hifadhi,
lakini yeye hakai katika bonde kutokana na mazingira ya malisho yake- hakuna
miti mirefu na kutokana na shingo yake kuwa ndefu hawezi wakati wote kuinama
kutafuta malisho lakini pia aina ya majani ambayo mnyama huyo hupendelea kula
nakakosekana katika bonde la Ngorongoro.
Swala au
Mbuzi pori kama ajulikanavyo na wengi, pia hayuko katika bonde hilo kutokana na
ukweli kwamba yeye hupenda kuishi katika vichana jambo ambalo haliko katika
bonde hilo.
Wanyama wengi
hupata maji katika mto mmoja tu uliopo katika bonde la Ngorongoro ujilikanao
kama Munge.
Nyumbu ni
mnyama mwenye sifa ya pekee, kwanza ndio walio wengi katika mbuga, wapole,
wanaonewa sana na wanyama wanaokula nyama lakini kikubwa ni kwamba mtoto wa
Nyumbu akizaliwa, ana uwezo wa kukimbia kwa spidi ya mama yake ndani ya dakika
10.
Kinachovutia
zaidi ni kuona wanyama wote, wakali na wapole jinsi wanavyoishi kwa pamoja hadi
pale tu wanapokuwa na njaa ndio hubadilikianana. Penye kundi la Nyumbu, Faru,
Punda milia, Ngiri, Nguruwe na kadhalika utawakuta pia Simba pembeni wamelala
wakipunga upepo baada ya kupata mlo wa mchana. Hii ni kuonyesha kwa jinsi gani
wanaishi kama familia moja na wako katika nyumba moja.
Tofauti iko
kwa Nyati. Mara nyingi mnyama huyu huwa hana urafiki na wanyama wengine
wanaokula majani kama wao. Mara nyingi utawakuta wao wako kwa umbali mdogo
kutoka walipo wanyama wengine.
Siku za utoto
wangu nilikuwa nikiamini kuwa ndege mkubwa ambaye huruka ni Tai. Lakini kwa
maajabu ya Ngorongoro yuko ndege mkubwa na mzito ambaye huruka kama
tai.
Hifadhi ya
Ngorongoro yenye ukubwa wa kilometa 210 inastahili sifa zote za kuwa miongoni
mwa maajabu saba duniani. Ni mahali ambapo mbali ya kuona wanyama mbalimbali
hususan faru weusi ambao huogopewa kwa ukali, Tembo wakubwa wazee na ndege aina
ya ‘Flamingo’, pia kuna hali ya hewa ya pekee ambayo inavutia kuishi hasa kwa
watu wasiopenda mazingira ya joto kali.
Wadau wa
sekta ya Habari nchini wakiwa katika Hifadhi ya
Ngorongoro.
Picha juu
na chini Baadhi ya wadau wa sekta ya Habari waliopata nafasi ya kutembelea
Hifadhi ya Ngorongoro katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani iliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment