June 18, 2014

  • NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KANDA YA ZIWA



    NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KANDA YA ZIWA

    Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), lahitimisha   kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya Ziwa.

    Lengo la kambi hizi zilikuwa ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

    Zoezi ambalo lilianzia mkoa wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 na kufuatiwa na mkoa wa Shinyanga hususani wilaya ya Kahama ambako walijitokeza watu 700, Mkoa wa Geita ambako watu1000 walijitokeza, litahitimishwa kwa kupima wakazi wa Mkoa Kagera wilaya ya Bukoba Mjini  , kwenye Viwanja vya Mashujaa (Platform),  kuanzia tarehe 14/06/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.

    HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
    Huduma mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;
      Upimaji wa Shinikizo la damu
    Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
    Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
    Utoaji wa dawa za Minyoo
     Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
    Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
      Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

    Huducma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

    Pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu kwa hiyari kwenye kambi hii ya Bukoba ambalo litaendeshwa na chama cha msalaba mwekundu.

    NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. 

    NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda, Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

    Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

    Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

    NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
    Banda la NSSF.
    Maofisa wa NSSF wakisikiiza kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa Ufunguzi wa Kambi ya upimaji Afya Bukoba.
    Meza kuu wakifurahi wakati wimbo wa mkoa wa Kagera ukiimbwa. Toka Kushoto, Dr.Ruta Thomas, Mganga Mkuu mkoa wa Kagera, Bw.Adoh Mapunda ,Mkurugenzi wilaya ya Bukoba, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bw.Leornard Faustine Kachebonaho, Mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu , Kagera . Dr.Ali Mtulia Meneja wa Mafao ya Matibabu –SHIB na Mratibu wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoa wa Kagera, Bi.Robi Wambura.
    Mkuu wa mkoa Kanali Mstaafu Fabian Massawe akisisitiza jambo wakati wa risala yake ya ufunguzi.
    Dokta Ali Mtulia, Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, watatu toka kushoto, Huku Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dr.Ruta Thomas(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa wilaya ya Bukoba, Bw.Adoh Mapunda(wa pili Kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Kagera , Bw.Leonard F Kachebonah0 (wan ne toka kushoto) wakisikiliza kwa Makini.
    Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe (katika), akikagua mabanda wakati wa zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.
    Ofisa Uhusiano Jumanne Mbepo akimkabidhi Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe vipeperushi na Fulana alipotembelea banda la kutoa elimu kwa umma juu ya NSSF.
    Wakazi wa mkoa wa Kagera wakijiandikisha kwa ajili ya kupima afya.
    :Dokta  Ali Mtulia akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe aweze kukagua mabanda yanayotoa huduma za upimaji.
    Dokta Ali Mtulia akimuelekeza Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu, Fabia Masawe upimaji wa Uzito na Urefu ili kutambua uwiano wa uzito na urefu kwa lengo la kushauri lishe bora.
    Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe, akiuliza maswali na kujibiwa na Dk.Ali Mtulia kuhusu huduma zitolewazo na NSSF.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.