May 19, 2014

  • Semina Sekta ya Pamba yafanyika Dar



    Pamba
    Mfadhili Mh. David Sainsbury wa Taasisi ya Gatsby Charitable Trust iliyopo nchini Uingereza.
    Na Mwandishi wetu
    Taasisi ya Tanzania Gatsby Trust (TGT) chini ya Programu ya Maendeleo ya Pamba na viwanda vya nguo (CTDP), hivi karibuni wameandaa semina kwa sekta ya pamba nchini yenye lengo la kupitia upya mafanikio, changamoto zilizojitokeza na maazimio yatakayo kuwa yamezingatiwa.
    Semina hiyo pia iliwapongeza wasindikaji na viongozi wa Wilaya kutokana na kuweza kuendeleza mazingira bora ya uwekezaji katika kilimo cha mkataba katika baadhi ya wilaya na baadhi ya maeneo, na kutambua kuwa uongozi mzuri na mbinu bora za biashara vinachangia kuongeza tija kwa zao la pamba nchini Tanzania. Pia ni fursa ya kuipitia upya sekta hiyo na kutambua nini kimefanyika kuhakikisha inaendeshwa kisasa.
    Semina hiyo itaudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wasindikaji wa zao la pamba, Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Christopher Chizza,  Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Taasisi ya Tanzania Gatsby Trust (TGT) na Mfadhili Mheshimiwa David Sainsbury wa Taasisi ya Gatsby Charitable Trust iliyopo nchini Uingereza.
    Mheshimiwa Sainsbury anatambua na kuthamini kile ambacho Mheshimiwa Chiza amekifanya kutokana na changamoto ambazo amekumbana nazo kwenye sekta hiyo ambayo inahitaji mageuzi makubwa.
    “Hoja ya kuanzisha kikosi kazi katika Wizara yake kuweza kuangalia masuala ya sera ya bei, mageuzi ya CDTF, utendaji bora wa kilimo cha mkataba kilimo na mageuzi kwenye TACOGA yanahitajika kwa wadau na washirika.” alisema Bw. Sainsbury.
    Inakadiriwa kuwa kati ya mara 2-3 ya wakulima wengi wataweza kupata pembejeo kupitia wasindikaji  ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa mfano karibu wakulima 88,000 mwaka 2013-14 ikilinganishwa na 30,000 kwa msimu uliopita.
    Bw. Sainsbury, alisema kuwa inaonekana kwamba uzalishaji kwa ujumla utaongezeka na hasa katika maeneo ambayo kilimo cha mkataba na matumizi ya mbegu zisizo na manyoya aina ya UK91 zimeshindwa.
    Kwa juhudi za pamoja msimu huu, kuwekeza kwa wasindikaji na uwekezaji kuwezesha mamlaka za wilaya kumetambua kilimo cha mkataba kama “njia yenye muelekeo.” Msimu huu tuna wilaya 18 na zaidi ya wakulima 1,000 waliopo kwenye kilimo cha mkataba, ikilinganishwa na misimu 8 iliyopita na wasindikaji 11 sambamba na zaidi ya wakulima 1,000 walio kwenye kilimo cha mkataba ikilinganishwa na misimu 8 iliyopita.
    Kuwekeza kwa wasindikaji huangalia utekelezaji wa kilimo cha mkataba kama mbinu ambayo huweza kupata usambazaji thabiti wa mbegu bora za pamba. Wasindikaji hawa wamebainisha usambazaji huu wa malighafi kama kitu muhimu kwa mafanikio yao na wako tayari kuwekeza katika mazingira ya biashara ambayo yana changamoto.
    Uwekezaji wa wasindikaji hawa umevutia  usawa wa maendeleo ya mamlaka za Wilaya na Mkoa ambao  wanaoona uwekezaji wa sekta binafsi katika uzalishaji wa pamba kama njia ya kuimarisha ustawi wa wakulima wa pamba na ule wa Wilaya kwa ujumla wake na kuimarisha ukusanyaji mapato kwa maendeleo ya jamii.
    “Serikali za mitaa zimekuwa kiungo muhimu katika sekta hii, na msaada wao hauna kipimo kwani wamekuwa wakitoa misaada kwa wasindikaji, wakulima na wadau wengine kuwahamasisha kuchukua njia bora katika sekta hii ya pamba na mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hii zinatokana na kujitolea,” alisema Bw. Sainsbury.
    Mafanikio ya kuongeza dhamira kwa mkulima kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa mbegu bora za pamba huongeza faida kwa wasindikaji wa sekta binafsi katika kutafuta na kuongeza faida ya uendeshaji kwenye uwekezaji wao nchini Tanzania; huongeza zaidi mapato ya wakulima wa pamba katika kutafuta kuongeza faida katika ardhi yao na kazi sambamba na kutoa maisha bora kwa familia zao na kuongeza ustawi wa wilaya kwa ujumla kwa njia ya kuongeza mapato katika wilaya na hivyo kupunguza ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa nafasi za huduma za umma.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.