June 20, 2014

  • Mtoto aliyezaliwa na mkia anayeabudiwa kama Mungu huko India.



    Mtoto aliyezaliwa na mkia anayeabudiwa kama Mungu huko India.
    Balaji3
    Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama Mungu na watu wa jamii yake.
    Balaji
    Arshid Ali Khan, mwenye miaka 13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake kutokana na mkia huo ingawa unamfanya aonekana kama alama ya uponyaji katika Jimbo la Punjab, India.Mtoto huyo anayetumia kiti cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.

    Balaji2
    Khan anasema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli.
    Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa tu.
    Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake wawili baada ya baba yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita na mama yake kuolewa tena.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.