Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery                    Silaa Wa Kwanza kulia  akifika eneo la  Tabata St                    Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho                    kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji                    safi na salama DAWASA.
         Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa                    Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa                    ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande                    cha barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida                    baina ya Mkandarasi na Dawasa
        Mkandarasi wa barabara ya                    Tabata-St Mary Bwana  George Lupia wa pili kutoka                    kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery                    Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi                    kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya                    barabara Hiyo.
        Meya wa Ilala Mh Jery Silaa                    akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya Tabata                    Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo                    kwenye mamlaka husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake                    ni Diwani wa Kata ya  Tabata St Marys Bi Mtumwa                    Mohamed mwenye Dira.
        Mkandarasi Geoge Lupia Akimwelezea                    Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia pesa                    nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa                    Barabara lakini kikwazo kimekuja baada ya kukuta                    mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza katikati ya                    barabara na pembeni Hivyo kuleta ugumu katika                    kufanikisha Umaliziaji wake.
        Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala                    Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa                    kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi                    ushirikiano wa kutosha na wa haraka katika                    kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
        Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala                    Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh                    Meya wa Ilala Jerry Silaa
        Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa                    Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini                    kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.
        Diwani wa Kata ya Tabata -St Mary                    Bi Mtumwa Mohammed Akielezea ni jinsi gani wanainchi                    wa eneo hilo wanapata tabu baada ya barabara hiyo                    kuchimbwa hivyo kufanya upitaji wa magari kusitishwa                    kwa mda eneo hilo
        Mkandarasi wa barabara ya                    Tabata_St Marys Bwana George Lupia akiongea na vyombo                    vya habari kuelezea ni ugumu gani anakumbana nao                    katika utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo,kutokana                    na mabomba ya Dawasco kupita katikati ya barabara Hiyo
         Hiki ndio kipande cha barabara ya                    Tabata-St Marys ambacho  kinashindwa  kuendelea na                    matengenezo kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita kati                    kati ya barabara na pembezoni,hivyo kumpa hali ngumu                    mkandarasi kuchimba eneo hilo ili ajaze kifusi.
        Pembenini maji yaliyotuama baada                    ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta usumbufu kwa                    mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.
         Hilo shimo hapo ni bomba amabalo                    limepita katikati ya barabara
         Mmiliki wa gari hii ndogo Toyota                    Premio alipatwa na hasira baada ya Gari yake kushindwa                    kupanda ili atokee upande wa pili ikambidi kushuka
         Kwa hasira mmiliki huyu akatoa                    vizuizi ya Barabara hiyo na kuvitupa pembeni
         Hapo mmiliki huyo akikagua gari                    yake kama imepata mikwaruzo
         Wakiendelea kutazama gari yao kwa                    umakini
        Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya                    vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.
        Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake.
Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.
Naye mkandarasi wa eneo hilo Bwana                    George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa                    ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita                    hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio                    akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea                    kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini                    hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao                    kuhamisha bomba hizo. 
        Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
0 comments:
Post a Comment