KOCHA wa timu ya taifa ya Holland, anajiandaa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United wiki hii na tayari amefichua kuhusu nahodha ajaye wa United.
Kiaina, Louis van Gaal aligusia kuwa Robin van Persie atakuwa nahodha wa Manchester United.
Akizungumza baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao dhidi ya Ecuador katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya Kombe la Dunia, Van Gaal alimwagia sifa nyingi Van Persie.
"Amecheza vizuri sana," alisema. "Alikuwa majeruhi lakini amerejea na kufunga bao tamu – ni ngumu kuamini – nilikuwa na furaha sana, lakini pia ni nahodha mzuri."
Alipotakiwa kufafanua zaidi, kocha huyo mwenye umri wa miaka 62, hakuficha utashi wake.
"Siku zote unamfanya mchezaji kuwa nahodha pale mnapofanana falsafa, sio kwaajili ya mbinu za soka tu, lakini pia ni kuhusu maisha," aliongeza.
"Kwahiyo nadhani hilo ni muhimu sana. Naamini mimi na Van Persie tuna falsafa zinazofanana."
Lakini Van Gaal bado aliendelea kukataa kuzungumzia juu ya kujiunga kwake na Manchester United kiangazi hiki. "Siwezi kusema lolote kuhusu hilo," aliongeza.
Kama kweli Van Gal ataikochi Manchester United na kumfanya Van Persie nahodha mpya, itakuwa ni habari mbaya kwa Wayne Rooney ambaye aliamini kabisa kuwa yeye ndiye nahodha ajaye Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment