July 18, 2014

  • Soma Taaarifa Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU-Zanzibar:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar na Israeli zina kila sababu za kuimarisha ushirikiano wao ambao wakati wote umeonesha mafanikio kwa kila upande.




    Soma Taaarifa Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU-Zanzibar:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar na Israeli zina kila sababu za kuimarisha ushirikiano wao ambao wakati wote umeonesha mafanikio kwa kila upande.

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
    ---
    STATE HOUSE ZANZIBAR
    OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
     
    Zanzibar      18 Julai, 2014

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar na Israeli zina kila sababu za kuimarisha ushirikiano wao ambao wakati wote umeonesha mafanikio kwa kila upande.

     Akizungumza na Balozi wa Israeli nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mheshimiwa Gill Haskel, Dk. Shein alisema ushirikiano kati ya Zanzibar na Israeli umeshuhudia matokeo mazuri hususan katika sekta za afya na kilimo.

     Alieleza kuwa chini ya ushirikiano huo Israeli imekuwa ikisaidia matibabu kwa watoto wenye matatizo ya afya kupitia Mpango wa Huduma ya Afya kwa Watoto ambapo hadi sasa watoto zaidi 200 hasa wenye matatizo ya moyo wamefaidika na mpango huo.

     Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ingependa kuona ushiriki zaidi wa Israeli katika kuunga mkono mpango wa Serikali kuimarisha kilimo hasa katika kuwajengea uwezo watafiti wa Zanzibar na kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo nchini.


     Alifafanua kuwa chini ya mpango huo wa Serikali, moja ya lengo ni kujitosheleza kwa chakula kwa kuongeza uzalishaji kupitia uimarishaji wa kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya mbinu za kisasa za kilimo.

     Aliongeza tangu kuanza kwa mpango huo uzalishaji katika kilimo cha mpunga umeongezeka mara tano hivyo lengo la kufikia angalau asilimia 50 ya mahitaji ya chakula ifikapo mwaka 2015/2016 linaelekea kufikiwa.

     Sambamba na kilimo cha mpunga Mheshimiwa Rais alimueleza Balozi huyo kuwa fursa pia zimeelekezwa katika kuwasiaidia wakulima katika mazao mengine ikiwemo kilimo cha mbogamboga zikiwemo tungule asili ambazo zinalimwa maeneo kame.

     Mheshimiwea Rais alitumia fursa hiyo pia kuiomba Serikali ya Israel kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na maafa yakiwemo katika usafiri wa majini.
     Alibanisha kuwa Zanzibar inahitaji kuwa na vifaa na utalaamu kujiandaa na kukabiliana na maafa ili kupunguza vifo na upotevu wa mali maafa yanapotokea.

     Kwa upande mwingine Dk. Shein alimueleza Balozi huyo fursa zilizopo katika sekta ya utalii Zanzibar kueleza matumaini yake kuwaBalozi huyo atatumia fursa ya kuwepo wake Tanzania kuzitangaza fursa hizo kwa wananchi wa Israeli kuwekeza na kuja Zanzibar wakiwa watalii.
     Aliongeza kuwa hivi sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya jitihada kuitangaza Zanzibar katika masoko ya Utalii ya China na Bara Asia ambapo kwa sasa ni watalii wachache kutoka sehemu hizo za dunia hufika Zanzibar.

     Alimueleza Balozi huyo kuwa mbali ya vivutio vilivyoko,sifa nyingine kubwa ya  Zanzibar ni ukarimu wa watu wake na wakati wote ni salama na tulivu.

     Kwa upande wake Balozi Gill Haskel ambaye alikuwa amefuatana na mke wake alimhakikishia Mheshimiwa Rais juu ya azma ya Serikali ya nchi yake ya kuendeleza ushirikiano na misaada yake kwa Zanzibar.

     Alieleza kuwa anaondoka huku akiwa anaamini kuwa katika kipindi chote alipokuwa akiitumikia nchi yake humu nchini ameweza kuimarisha uhusiano kati ya Israel na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

     Aliongeza kuwa anahakika kuwa Balozi ajaye sio tu kuwa ataendeleza na kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya ushirikiano yaliyopo sasa bali pia ataangalia uwezekano wa kupanua maeneo mapya yakiwemo hayo aliyayagusia Mhehimiwa Rais wakati mazungumzo yao.

    Balozi Gill Hakel amemueleza Mheshimiwa Rais kuwa milango iko wazi kwa Zanzibar kujifunza mafanikio ya nchi yake katika nyanja mbalimbali kwa kutumia fursa zinazotokana na ushirikiano wake na nchi hiyo.

    Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.