May 19, 2014

  • SAUT MABINGWA SPORTS XTRA DAY 2014 MKOA WA MWANZA.



    Mabigwa wa Sports Xtra Day 2014 mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya NMB Mwanza, ambapo SAUT walitawazwa kuwa mabingwa mara baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5 - 4.
    BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA.

    Washindi nafasi ya pili NMB Mwanza katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na SAUT.
    Kandanda safi la kuvutia limeonekana katika mchezo wa fainali kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa kuepuka makosa kiasi kilichosababisha mchezo huo kuamriwa kwa mikwaju ya penati ambapo SAUT walitawazwa kuwa mabingwa mara baada ya kushinda kwa mikwaju 5 - 4 dhidi ya NMB Mwanza.
    Patashika langoni mwa NMB Mwanza.
    Kasi, ufundi, umakini vimevuta hisia za mashabiki viwanja vya Raila Odinga Chuo cha SAUT Mwanza katika michuano ya Bonanza la Sports Xtra kwa mkoa wa Mwanza.
    Patashika langoni mwa SAUT pale ambapo NMB Mwanza walipo lishambulia kama nyuki.
    Kasi kuuwania mpira.
    Mashabiki wengine hakuna kukaa mwanzo mwisho.
    Jiografia ya ground husika.
    Macho ya mashabiki kwenye mchezo waupendao.
    Dakika za mchezo zilimalizika na sasa mikwaju ya penati ndiyo mpango mzima hapa mchezaji wa SAUT alifanikiwa kuutumbukiza mpira kimiani.
    Hamasa ya wachezaji wa NMB Mwanza wakati wa mikwaju ya penati dhidi ya SAUT mchezo wa fainali ya Bonanza la Sports Xtra Day 2014 lililofanyika leo 18/05 katika viwanja vya Raila Odinga jijini Mwanza ambapo SAUT walitawazwa kuwa mabingwa mara baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5 - 4.
    Penati ya akili sana toka kwa mchezaji wa NMB Mwanza.
    Sehemu ya mashabiki na macho kwenye mchezo waupendao (SOKA).



    Ni mashabiki wa Chuo cha SAUT Mwanza wakiwa wamembeba golikipa wao aliye pangua penati ya mwisho ya nahodha wa NMB Mwanza Hassan Mtalemwa.
    "SAUT, SAUT, SAUT" ndiyo wimbo unaosikika hapa.
    Father Leons Maziku ametoa shukurani kwa Clouds Fm kupitia Sports Xtra kuandaa Bonanza la Sports Xtra Day kwani limesaidia kukutanisha watu muhimu toka viwanda, makampuni na mashirika mbalimbali ambayo yameshiriki na mwisho wa siku yametengeneza Fursa ya Network (mawasiliano) si kwa makampuni na mashirika pekee bali pia Network kwa wafanyakazi watarajiwa ambao ni wanachuo.
    Meneja wa masoko kanda ya ziwa Kampuni ya Mega Trade James Edward Njuu amesema kuwa huu ni mwanzo tu kwa kampuni yake kushiriki Bonanza hilo, kampuni yake imepania kuelekea Mbeya mwishoni mwa wiki ijayo ili kushiriki halikadhalika Arusha ambapo kiwanda cha utengenezaji wa vinywaji kama K Vant, Kiroba Original  toka kampuni yake kipo mjini humo.  
    SAUT na kombe  lao la ubingwa Bonanza la Sports Xtra Day 2014 Mwanza.
    Mashabiki wa NMB Mwanza pamoja na baadhi ya wachezaji hawakusita kushangilia eti kisa kufungwa fainali, tena kwa makusudi walimbeba nahodha wao Mtalemwa akiwa na kombe la nafasi ya pili.
    Mbwiga wa Mbwiguke (wa pili kutoka kushoto) akiwa na mashabiki wake.
    Kikosi cha Sports Xtra kilichoenguliwa kwa taaaaaaaaaabu katika mchezo wa nusu fainali kwa njia ngumu ya mikwaju ya penati 2 - 3 dhidi ya NMB Mwanza. 
    Kikosi cha VODACOM Mwanza licha ya kuonyesha soka tamu la kuvutia kiling'oka katika ngazi ya nusu fainali kwa penati 4 - 5 dhidi ya SAUT.
    Kikosi cha washirika wengine muhimu sana kwenye Bonanza la Sports Xtra Day 2014 Mwanza Advans Bank.
    Kikosi cha washirika wa karibu sana moja kati ya wadhamini wa kipindi cha Sports Xtra Clouds fm, Tigo Mwanza katika picha ya pamoja.
    Mwisho ilikuwa ni kujipongeza kwa kupata msosi makini huku tukiwa na nyuzi za Binslum.
    Shukurani za kipekee kwa NMB Mwanza, VODACOM, MEGATRADE, TIGO, Chuo cha SAUT, Songora Marine Services na Advans Bank kwa kushiriki Sports Xtra Day Mwanza, tukutane tena mwakani . 
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.