Karama Nyilawila na Said Mbelwa wakionesha mkanda wao watakao gombania. |
Karama Nyilawila ni bondia
anayetegemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 may kuzichapa na Said Mbelwa
kuwania ubingwa wa UBO (Universal Boxing Organisation) katika ukumbi wa Friends
corner – Manzese.
Hapo awali karama alikuwa azipige na
Thomas mashali alievunja mkataba wa pambano kwa kutokuwa vema kwa pambano hilo
na badala yake nafasi hiyo ikadondokea kwa said mbelwa ambaye ana vigezo vyote
vya kugombania ubingwa.
Khalid Chokoraa akiwa mazoezini. |
Karama Nyilawila akiwa katika mazoezi
ya mwishomwisho alisema” Mashali ananiogopa baada ya kusikia mazoezi ninayofanya
ni magumu na hatari kwa bondia atakae katiza mbele yangu, kwani kila siku
asubuhi lazima nikimbie kutoka sinza ilipo gym yetu mpaka kibaha maili moja
kwenda na kurudi na jioni napiga mfuko wa mazoezi(bag) raundi sita za dakika
kumikumi na nacheza sparing raundi 15, aliposikia hivyo mdogo wangu mashali
ikabidi achomoe kwa kutafuta visingizio mbalimbali na pambano limekuwa
likibadirishwa tarehe kwa ajili yake na mwishowe akaweka wazi kuwa
ananiogopa.
Karama aliendelea kwa kusema huyu
Mbelwa kavamia adhabu ambayo sio yake,asuburi tarehe ifike apate cha
kumuhadithia mashali.
Nae kiongozi na mratibu
wa pambano hilo Ibrahim kamwe amesema siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi
makali ya utangulizi yakiwemo ya Suleiman Tall akizipiga
na Abdala Pazi, Ramadhan Kumbele akimvaa morobest, Zumba Kukwe wakioneshana
ubabe na
kamanda wa makamanda, idi athuman na Julias
Kisarawe.
Khalid Chokoraa akiwa ktk pozi. |
Wakati huohuo ndio
tunamalizia makubaliano ya mwisho ya bondia chipukizi na
mwanamuziki mashuhuri wa bendi ya
mapacha watatu Halid Chokoraa ambae amekubali kuzipiga na Abdul Manyenza katika
pambano la raundi nne kilogram 63. Chokoraa kwa sasa yupo vizuri sana kwa mchezo
wa ngumi na ana uwezo wa kumkabili bondia yoyote wa uzito
wake.
0 comments:
Post a Comment