Na Pascal Mayalla
Ziara
ya Meli za Jeshi la Uturuki Nchini Tanzania. Meli Nne za Kijeshi za
Uturuki kwa jina la Barbaros Turkish Maritime Task Group (TMTG)
zinatarajiwa kutia nanga kwa wakati mmoja katika Bandari ya Dar es
Salaam kwa ziara ya kijeshi ya siku 4 ambao itahusisha maonyesho ya zana
za kijeshi, mazoezi ya pamoja na jeshi la wanamaji la Tanzania, huduma
za kijamii na ushirikiani wa kijeshi baina ya Uturuki na Tanzania.
Hayo
yamebainishwa jiji Dar es Salaam na Balozi wa Uturuki nchini, Ali
Dovitoglu katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ubalozi wa
Uturuki, jijini Dar es Salaam.
Balozi
Dovitoglu amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kukuza ushirikiano wa
kijeshe baina ya jeshi la Uturuki na majeshi ya nchi 27 za pwani barani
Afrika sio tuu kuonyesha uwepo na uwezo wa kijeshi wa Jeshi la Wanamaji
la Uturuki, bali pia kusaidia katika operetions mbalimbali za kijeshi
barani Afrika ukiwemo vita dhidi ya uharamia kwa Pwani ya Bahari ya
Hindi.
Balozi
Dovitoglu amesema meli hizo zitawasili siku ya Jumanne tarehe
27/05/2014, Siku ya Jumatano, tarehe 28/05 2014 waandishi wa habari
watakaribishwa kufanya ziara katika meli hizo, baadaye wanamaji hao,
watatembelea shule na kituo cha watoto yatima kugawa misaada ya
kibinaadamu.
Siku
ya Alhamisi na Ijumaa, wananchi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji
vyake, wataruhusiwa kutembelea meli hizo kwa muda wa siku 2 kuanzia saa 3
asubuhi mpaka saa 6 mchana kujionea maonyesho ya zana za kijeshi ya
Uturuki ambapo makampuni manane ya vifaa vya kijeshi ya Uturuki
wataonyesha vifaa vyao.
Makampuni hayo ni Meteksan, Otokar, TAI, Dearsan, Havelsan, Roketsan, Aselsan na STM
Meli
hizo nne ni F-495 TCG kwa jina la Gediz, F-245 TCG, Oruçreis, F-511
TCG Heybeliada meli ya usindikizaji ya A-595 TCG Yarbay Kudret Güngör,
zitasafiri kwa jumla ya safari ya urefu wa kilometa 30,000 katika ziara
itakayochukua siku zaidi ya 100 ambapo itatembelea nchi 28 barani Afrika
na kutia nanga katika bandari 40.
Msafara
wa meli hizo, unaingia Tanzania ukitokea nchini Afrika ya Kusini,
ambapo hii ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 148 iliyopita
ndipo meli ya mwisho ya Uturuki ilitia nanga kwa mara ya mwisha katika
Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope) mwaka 1866.
Uturuki
ni moja ya mataifa makubwa yenye nguvu kubwa za kijeshi la la majini,
tangu enzi za utawala wa kale wa dola la Ottoman ambapo walitawala
bandari nyingi barani Afrika ikiwemo miji ya Kilwa, Sofala, na Lamu
kwatika Pwani ya Bahari ya Hindi. Mwisho.
na
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu katika mkutano na waandishi wa
habari, uliofanyika Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es Salaam
na
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu akihojiwa na mwandishi wa ITV
Bi. Fatuma Almasi Nyangassa kwenye Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es
Salaam
0 comments:
Post a Comment