August 18, 2014

  • KILWA WAENDELEA KUFAIDI HUDUMA ZA WAWEKEZAJI WA GESI


    KILWA WAENDELEA KUFAIDI HUDUMA ZA WAWEKEZAJI WA GESI
    Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mchango uliotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kutoka kwa Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki .

    Na Abdulaziz Kilwa Masoko

    Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wameendelea kunufaika na wawekezaji,baada ya kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kuikabidhi halmashauri hiyo zahanati ya kijiji cha Nangurukuru ambayo ujenzi wake umegharimu Tshs 262 Milioni .

    Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalifuatiwa na utiaji sahihi mkataba wa ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo ujenzi wake hadi kukamilika utagharimu shilingi 458 milioni Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki alisema katika ujenzi wa zahanati hiyo kampuni ya PANAFRICA N imechangia jumla ya shilingi 216,000,000.

    Ambapo pia kutokana na tatizo la wafanyakazi pia kampuni imeamua kufadhili ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo mkataba wenye thamani ya shilingi 458,000,000 ulisainiwa baina ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw David Roberts na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi zahanati.

    Aidha Kashangaki alibainisha kuwa sera ya kampuni hiyo licha ya kufanya kazi ya uzalishaji wa Gesi ya songosongo pia hutoa misaada kwa jamiii ikiwemo kufadhili programu ya ufundishaji lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za halmashauri hiyo,ambapo jumla ya shule za sekondari 20 kati ya 28 zimenufaika na programu hiyo.

    'Wana kilwa tulianza kusaidia elimu ya kiingereza kwa kuzifikia shule 20 ila kwa umuhimu wa elimu kuanzia mwakani tutazifikia shule zote 28 za sekondari ikiwemo kusaidia upatikanaji wa Umeme Jua kwa shule ambazo hazina umeme 'Alimalizia Kashangaki.

    Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega licha ya kuishukuru kampuni hiyo aliwataka wananchi kupuuza kauli zinazosemwa ikiwemo baadhi ya Vyombo vya habari kupotosha na kudai Manufaa ya Gesi yapo katika kijiji cha Songosongo pekee Na kubainisha baadhi ya maeneo yanayonufaika ikiwemo hapo Nangurukuru,Njinjo ,Somanga na kilwa masoko

    'Wananchi wa Kilwa nadhani ni mashahidi kampuni hii imesaidia wilaya yote si Kama Gazeti moja lilivyoandika hivi karibuni Huu ni upotoshaji mkubwa kwani elimu inasaidiwa wilaya yote,Afya Hivyo hivyo,Maji wananufaika mpaka Njinjo na hata mrahaba unaolipwa na kampuni hiyo zaidi ya Nusu inachangia katika sekta ya elimu Tuwe makini kuyajua haya yenye ukweli si maneno tu ya vijiweni...Alimalizia Ulega.

    Awali akifungua hafla hiyo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nangukuru,Hamis Ligweje alisema kabla ya PANAFRICAN kufadhili ujenzi huo,wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wahisani wengine ikiwamo shirika la Action Aid walichangia walichangia jumla ya shilingi Milion 46 ujenzi ambao ulikuwa wa kusuasua mpaka wahisani hao walipojitokeza kusaidia kuikamilisha.

    'Hakika tulishindwa kabisa na Tulifikia hatua ya Kumuomba Rais Kikwete Kusaidia alipokuja katika ziara yake ambapo aliwaagiza Viongozi wa Wilaya kuangalia uwezekano ndipo Mkurugenzi aliehama Bw Mapunda Alifanikisha kuwaomba hawa wahisani na leo wametukamilishia na tunafarijika zaidi walipoamua kutujengea na Nyumba 2 kwa 4 za watumishi itasaidia sana si kwa Nangurukuru tu hata wasafiri watakaopata dharula katika barabara kuu.

    Licha ya kukabidhi Zahanati hiyo Mkurugenzi mkuu wa Pan African Energy,David Roberts Alikabidhi Vitanda Viwili vya kujifungulia akina mama ikiwa ni hatua ya awali ya kuokoa Akina mama katika suala la Uzazi.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.