JAJI katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius wa Afrika Kusini anasema kuwa mwanariadha huyo lazima aanze kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa muda wa mwezi mmoja kubaini hali yake kiakili alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Jaji Thokozile Masipa aliamuamuru Pistorius kua awe anakwenda katika hospitali ya maradhi ya kiakili ya Weskoppies mjini Pretoria kila siku kuanzia tarehe 26 mwezi Mei.
Amri ya jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na kuwa na wasiwasi wakati wote.
0 comments:
Post a Comment