May 20, 2014

  • Nimetongozwa na Shoga la Kiume Kwenye Daladala

     
    Siku ya jana nimekutana na mkosi wa aina yake ilikuwa mida ya saa 7 mchana nikitoka Sinza kuelekea Posta kufanya yangu .
     
    Ndipo daladala ilipofika maeneo ya Magomeni alipanda jamaa mmoja kiukweli daladala haikuwa na abiria wengi kwani kulikuwa na siti za wazi nyingi na mimi nilikaa mwisho kabisa wa daladala cha ajabu na kilichonishangaza jamaa kaacha siti zote kaja kukaa na mimi akasema samahani kaka siti za mbele huwa sizipendi huku anachekacheka.
     
    Akaanza kuniuliza kila kituo tukifika eti hapa ndo wapi,Maria leo fire foleni hamna,mara nimechelewa kazini nikifika tu navaa unform haraka alivyoona niko kimya akasema kaka vipi mbona we mpole hivyo nikajichekesha kidogo nikamwambia kawaida tumefika Jangwani akaanza kunitongoza kaka unaitwa nani,unaishi wapi,we ni last born nini umepanga au unaishi kwa wazazi alafu umependeza,nataka uwe mume wangu pesa ninazo.
     
    Kiukweli uzalendo ulinishinda nilijikuta ninemfokea kwa nguvu na kumtusi matusi ya maana sijui hata yalipotoka hayo matusi aibu ilimjaa sana jamaa ikawa habari ndani ya daladala.
     
    Ilinibidi nishuke kituo ambacho sikupashwa kushuka,watu wengine mikosi sana.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.