LEWIS Baker alikuwa shujaa wakati Chelsea ilipotoka nyuma na kuichapa Manchester United 2-1 na kunyakua kombe la Premier League kwa vijana chini ya miaka 21.
Katika fainali hiyo iliyopigwa Old Trafford, kiungo huyo wa Chelsea alifunga bao la ushindi dakika ya 79 akitumia vizuri mwanya ulioachwa na mabeki wa United na kuuchonga mpira uliompita kipa Ben Amos.
LEWIS Baker akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi
Lilikuwa ni moja kati ya mabao matatu matamu yaliyofungwa katika fainali hiyo iliyowaburudisha vilivyo watamazaji 13,000.
United ambao walikuwa wanatetea taji lao, walifunga bao la mapema kupitia kwa Tom Lawrence kunako dakika ya 12.
TOM Lawrence furahani baada ya kuifungia bao United
Chelsea wakasawazisha dakika 10 baadae wakati Mbelgiji hatari Charly Musonda alipowafungisha tela mabeki watatu wa United na kuachia shuti la chini chini lililotinga wavuni.
Manchester United: Amos; Varela, McNair, M Keane, James (Blackett 81); Janko, Ekangamene, Pearson, A Pereira, Lawrence (Harrop 84); Wilson (Weir 67)
Chelsea: Blackman; Ssewankambo, Aina, Christensen, Nditi; Loftus-Cheek (Palmer 77'), Baker, Ake; Swift, Feruz, C Musonda (Colkett 85')
NYWELE hewani: Ben Pearson (kushoto) na Nathan Ake wa Chelsea katika heka heka nzito
MAKOCHA Paul Schoes na Giggs wakitazama jahazi lao la United likizama
HUZUNI: United wakiangalia Chelsea wanavyokabidhiwa kombe
0 comments:
Post a Comment