LAANA ya kocha wao wa zamani Bela Guttmann inaendelea kuwaandama Benfica ya Ureno baada ya kufungwa kwa matuta na Sevilla ya Hispania kwenye fainali ya kombe la European.
Timu hizo mbili zilitoshana nguvu kwa sare ya 0-0 hadi dakika 30 za 'extra time' na kulazimika kupigiana mikwaju mitano mitano ya penalti ambapo Sevilla ikaibuka kijogoo kwa 4-2.
Benfica, timu iliyotandaza soka tamu kwa dakika 120 ikajikuta inapata mpasuko wa moyo kwa mara ya nane mfululizo kwenye fainali ya European Cup.
Mshambuliaji wao mkongwe Oscar Cardozo na Rodrigo walikosa penalti wakati Sevilla walidumbukiza wavuni mikwaju yao yote minne.
Baada ya kushinda mataji ya Ulaya na Benfica mwaka 1962, Bela Guttmann alitimuliwa kufuatia mgogoro wa malipo na kocha huyo aliapa kuwa timu hiyo haitashinda taji lolote kwa miaka 100 ijayo.
Mwaka jana walipigwa na Chelsea katika fainali ya michuano hii, na mwaka huu mambo yamekwenda hivyo hivyo.
0 comments:
Post a Comment