Mtoto Sauda Mohamed aliyeokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake.
MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika.
Habari zinasema mtoto huyo baada ya kuokotwa alifikishwa katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala ambako alipokelewanakulelewa.ALIVYOOKOTWASauda aliokotwa na msamaria mwema maeneo ya Buguruni sehemu ya wazi akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye hajafahamika.
Chanzo chetu kilisema mara baada ya kuokotwa taratibu zilifanyika kwa kumfikisha Kituo cha Polisi Buguruni kisha akapelekwa moja kwa moja katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo, Dar.
Akifafanua kuhusu tukio hilo mkurugenzi wa kituo hicho, Mwanaisha Magambo alikuwa na haya ya kusema: "Sauda aliokotwa akiwa na umri wa miaka mitatu hata hivyo, walifanya vipimo vya kitaalamu ili kujua umri kwa kumpima kichwa na baadhi ya viungo vya mwili wake.
"Alipookotwa alikuwa na hali mbaya sana kipindi hicho kwani alilazwa mwezi mzima katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapumlia mashine na mapigo ya moyo yalikuwa juu sana.
AGUNDULIKA MATUNDU KATIKA MOYO
"Kutokana na kuwa na hali mbaya, madaktari pale Muhimbili baada ya vipimo wakagundua kuwa ana matundu "Baada ya kugundulika tatizo alipewa dawa za kutumia na akaruhusiwa lakini hali ilibadilika na ikalazimu arudishwe tena Muhimbili ambako amelazwa."
Mtoto Sauda Mohamed akiwa amelala.
MAANDALIZI YA SAFARI YA INDIA
Magambo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo Sauda hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea, akitaka kusogea huwa anatambaa."Mbaya zaidi ugonjwa huo umemfanya Sauda asiwe na uwezo wa kusema na mwili wake umedhoofu ikiwemo miguu.
"Kuna maandalizi yanafanywa ili apelekwe India kwa matibabu zaidi kutokana na ukweli kwamba tatizo lake ni kubwa maana sasa hata kula hawezi," alisema.
Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, mlezi wa mtoto huyo, Bi. Magambo alisema amefariki dunia na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar.
WITO KWA WAZAZI
Tunapenda kutoa wito kwa wazazi kwamba si vema kutupa watoto. Matatizo ya Sauda yalichangiwa kutokana na kutupwa na mzazi wake, hivyo kukumbwa na maradhi lukuki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina- Mhariri.
0 comments:
Post a Comment