ARSENAL itaangalia uwezekano wa kumpata mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzima mara tu baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akiwindwa na Wenger kwa miaka kadhaa ambapo Arsenal ilishindwa kumsajili mshambuliaji huyo katika vipindi viwili mfululizo vilivyopita vya majira ya kiangazi.
Arsenal wako tayari kujaribu tena kupata saini ya Benzima kiangazi hiki, ikiwa imedhamiria kuimarisha kikosi chake kwa kumpata mshambuliaji 'world class'.
Benzima amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake jambo linalodhihirisha kuwa ni lazima aidha ajadili mkataba mpya wa kukipiga Real Madrid au auzwe. Kinyume na hapo ni kwamba nyota huyo ataondoka bure mwishoni mwa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment