Serikali imetakiwa kutoa maelezo bungeni, kuhusu
sababu za kuuawa kwa waasisi sita wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
wanaodaiwa kuzikwa katika handaki moja Zanzibar.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano), msemaji wake, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza waasisi hao
walifanya makosa gani.
Aliwataja waasisi hao kuwa ni Abdallah Kassim
Hanga aliyekuwa Waziri Mkuu, Abdulaziz Twala aliyekuwa Waziri wa Fedha na Saleh
Akida aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na viongozi waandamizi wa Serikali
ya Mapinduzi, Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa ambao alisema waliuawa na
kuzikwa handaki moja eneo la Kama, Zanzibar.
Lissu alisema hayo huku akinukuu kitabu cha
‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’ kilichoandikwa na Harith Ghassany alichosema
kilionyesha jinsi viongozi hao walivyouawa na kuzikwa katika kaburi moja.
“Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua
ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na
kuzikwa katika kaburi au handaki moja,” alisema Lissu huku wabunge wakiwa kimya
kumsikiliza.
-Mtanzania
0 comments:
Post a Comment