MWIGIZAJI na mmoja wa waimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya, H-Baba (pichani), amesema soko la filamu Tanzania linaangamia kwa vile walio bora ndio wanaoondoka duniani.
H-Baba aliyasema hayo kufuatia kifo cha mwongozaji na mcheza filamu Adam Kuambiana aliyeiaga dunia Jumamosi asubuhi.
Akiongea na Saluti5 kwenye viwanja vya Leaders Club jana usiku, H-Baba alisema Adam Kuambiana alikuwa ni msanii bora katika nyanja zote kuanzia uwezo wa kisanii, ubunifu, lugha za kimataifa pamoja umahiri wake wa kuongoza kazi za wasanii wenzake.
H-Baba alisema: "Nadiriki kusema katika wacheza filamu waliobaki, hakuna wa kufikia kiwango cha Adam Kuambiana.
"Sisemi hili kwa kuwa amefariki, nimewahi kulisema mara kadhaa tangu akiwa hai. Adam alikuwa ni bingwa ila alikuwa anabaniwa.
"Lipo tatizo la kuwabana na kuwamaliza wasanii walio bora. Adam Kuambiana alikumbana na hali hiyo, kuna fursa zilifichwa kwa makusudi kwake, kuna milango ya neema ilifungwa kwake.
"Tazama filamu zote alizocheza Adam, utangundua kuwa aliwafunika wenzake hata kama alicheza sehemu ndogo ya filamu hiyo.
"Angalia 'Fake Pastors' aliyocheza mwaka 2007 akiwa bado hajulikani, lakini alimpoteza kabisa Ray ambaye tayari alishakuwa supastaa kwa kipindi hicho.
"Tazama filamu zote alizozindika na kuziongoza utangundua kuwa Adam ni habari nyingine."
H- Baba anasema kifo cha Kuambina ukijumlisha na kile cha Kanumba, ni ishara ya kudidimia kwa tasnia ya filamu hapa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment