BAADA ya kupotea kwa muda mrefu kufuatia ziara zao za mikoani, bendi ya FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" inajerea tena kwenye kiwanja chake cha kila Jumamosi.
Kuanzia Jumamosi hii Juni, 24, FM Academia watakuwepo Letasi Lounge (zamani Business Park) Victoria jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga ameiambia Saluti5 kuwa kuanzia Jumamosi hii na kila Jumamosi wataendelea kutumbuiza Letasi Lounge kama ilivyokuwa kawaida yao.
"Tulikuwa na ziara ya kuitangaza albam yetu "Chuki ya Nini" mikoani, lakini sasa tumerejea jijini," alisema Kelvin.
Kwa miezi kadhaa sasa, FM Academia imekuwa ikiutumia ukumbi wa Letasi kama ngome yao ya kila Jumamosi.
Aidha Kelvin alisema bonanza la kila Jumapili pale New Msasani Club linaendelea kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment