WAKATI mtandao huu ukipiga picha hizi pale Mango Garden Kinondoni Machi 27 mwaka huu, Saluti5 haikujua kama ndio ilikuwa inampiga picha kwa mara ya mwisho mwigizaji nyota Adam Kuambiana.
Adam Kuambiana alifariki ghafla jana asubuhi na kufanya picha hizi zilizopigwa kwenye onyesho la Mashauzi Classic ziwe ndio picha zake za mwisho kuingia kwenye maktaba ya Saluti5.
Inawezekana kabisa kuwa hata watu waliopiga picha hizi na Adam Kuambiana, pengine ndio picha zao za mwisho kupiga nae.
Hebu zitupie macho picha hizi pengine zinaweza zikakukumbusha kitu kuhusu safari ya binaadamu. Hakika kifo hakina hodi.
0 comments:
Post a Comment