MSANII Lucas Mhavile 'Joti'baada ya kukaa kimya kwa mda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika husika tofauti tofauti filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na Kampuni yaproin promotions ya jinini Dar es salaam.
Akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingini kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo aijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasinia hii ya filamu nchini.
Hivyo wapenzi wangu wakae mkao wa kula tu kwani wakati wowote kuanzia sasa itakuwa inaingia sokoni kwani filamu hii si yakukosa mana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey.
Hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala alisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee.
Mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka.'
Filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia luninga sasa ameludi tena katika filamu.
yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la joti sanduku la babu.
0 comments:
Post a Comment