BAYERN Munich wanajiandaa kupeleka ofa ya pauni milioni 25 kwaajili ya kupata sani ya beki wa kati wa Chelsea, David Luiz.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko tayari kuondoka Stamford Bridge kiangazi hiki.
Ilikuwa inaeleweka zaidi kuwa Luiz angependa kwenda Barcelona lakini hakuna dili lolote lililowekwa mezani na miamba hiyo ya Hispania huku baadhi watu wa benchi la ufundi la timu hiyo wakiwa hawana uhakika kama mchezaji huyo anapaswa kupewa kipaumbele katika nafasi ya mabeki wa kati.
Lakini kocha wa Bayern Pep Guardiola anamtaka Luiz kwa udi na uvumba.
Mazungumzo yanategemewa kufanyika baada ya Kombe la Dunia, hii inafuatia kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari kukataa wachezaji wake kubughudhiwa na mazungumzo ya usajili.
0 comments:
Post a Comment