May 15, 2014

  • BATULI WA BONGO MOVIE: SIJAWAHI KUPENDA KAMA NILIVYO MPENDA MTUNIS

     
     
     
     
    KWA mara nyingine, staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf  'Batuli' amemwaga data za kimapenzi akidai hajawahi kumpenda mwanaume kama alivyompenda Nice Mohammed 'Mtunis'.
    Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf  'Batuli'
    Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Batuli alisema licha ya kuwa walimwagana na staa huyo lakini hatokuja kupenda mwanaume kama alivyompenda Mtunis.
    "Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni mara moja tu mengine tutadanganyana," alisema Batuli.
    Hivi karibuni Batuli aliripotiwa kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha ajabu mtoto wa kike hakuonesha dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.