BARCLONA imevuliwa taji la La Liga kwenye uwanja wao wa nyumbani Nou Camp baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Hispania.
Wakiwa wanahitaji ushindi ili kutetea taji lao, Barcelona wakashindwa kulinda bao lililofungwa na Alexis Sanchez dakika ya 30 baada ya Diego Godin kusawazisha pale ilipotimu dakika ya 49.
Kwa sare hiyo, Atletico Madrid wamekuwa mabingwa wapya wa Hispania, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 18.
Kocha wa Barclelona Gerardo "Tata" Martino amesema anabwaga manyanga baada ya kuwa na msimu mbovu.
Kocha huyo anatimka akiwa ameikochi timu hiyo kwa msimu mmoja tu. Anasema yeye na Barcelona wamefikia muafaka wa kusimamisha 'kibarua' chake.
Wakati Tata anatangaza kubwaga manyanga, kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone anajiwekea historia ya aina yake baada ya kuipa ubingwa timu hiyo kama alivyofanya miaka 18 iliyopita akiwa mchezaji.
Wachezaji tegemeo wa Atletico Diego Costa na Arda Tura walitolewa kipindi cha kwanza baada ya kuumia. Costa alibubujikwa machozi kwenye benchi baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.
0 comments:
Post a Comment