June 20, 2014

  • PSPF NA BENKI YA POSTA WAZINDUA HUDUMA YA (WASTAAFU LOAN)



    PSPF NA BENKI YA POSTA WAZINDUA HUDUMA YA (WASTAAFU LOAN)
    1qMkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi na Mkurugenzi  Mkuu PSPF Adam Mayingu kulia wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya Wastaafu Loan mkopo unaotolewa na shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Posta kwa wastaafu, Kulia wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo na kushoto ni Muuguzi Mstaafu na RAS wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Eunice Temu, Uzinduzi huo umefanyika kwenye Jengo la PSPF lililopo Posta jijini Dar es salaam .2qKutoka kulia ni Muuguzi Mstaafu na RAS wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Eunice Temu, Mkurugenzi  Mkuu PSPF Adam Mayingu, Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo na Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi wakinyanyua mikono juu kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo.
    3qKatibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wastaafu wanaopata huduma ya Wastaafu Loan.4aKatibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo wa mashirika hayo.5qKatibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo katika picha ya pamoja na mameneja6qKatibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo maofisa mbalimbali wa mashirika hayo.7qKatibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akizungumza katika uzinduzi huo8aMkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu akizungumza na wageni waalikwa.9qMkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo.10qMsanii Mrisho Mpoto akifanya vitu vyake katika uzinduzi huo.11qWasanii wa Bendi ya Mjomba Band wakiigiza igizo la wastaafu wanavyohangaika katika mifuko mbalimbali ya Pensheni12qMaofisa mbalimbali wa mashirika hayo wakiwa katika uzinduzi huo.13qMaofisa mbalimbali wa mashirika hayo wakiwa katika uzinduzi huo.
    …………………………………………………………………….
    Leo Juni 20, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wastaafu ambao unajuliakana kama Wastaafu Loan, ambapo sasa wastaafu wa PSPF wanaweza kunufaika na mikopo hiyo.
    Lengo la mkopo huu ni kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji halisi ya fedha, na hatimaye kuboresha maisha yao. Miongoni mwa mahitaji makubwa ya fedha kwa wastaafu ni pamoja na gharama za matibabu, ada za shule, kuendesha biashara na miradi mbalimbali.
    kwa muda mrefu sasa hapa nchini taasisi mbalimbali za fedha zimekuwa hazitoi mikopo mbalimbali kwa wastaafu wakidhani kwamba wastaafu hawana uwezo wa kulipa, na kujenga dhana ya kutokopesheka, kwa kuliona hilo na kwa kutambua mchango wa wastaafu kwa taifa hili. PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania tumebuni mpango huu wa kipekee nchini wa kuwakopesha wastaafu wa Mfuko wa PSPF.
    Katika utafiti tuliofanya umeonesha kuwa wastaafu kwa ujumla wanaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha katika uchumi kutokana na mafao wanayolipwa. Mafao hayo yanaweza kuleta athari chanya (multiplier effect) katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kama vile kuongeza uwezo wa kifedha katika taasisi za kifedha, kuongeza ajira, kukuza kipato, kupunguza umaskini na kudumisha utulivu wa kisiasa nchini. Hili linawezekana iwapo fedha hizo zitatumika kwa busara na kuwekezwa katika maeneo salama. Ni wajibu wa PSPF kutimiza dhana ya kuwakinga wastaafu na majanga yote ya kiuchumi na ya kijamii yanayotokana na kupungukiwa na kipato. Kwa kuzingatia hili Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania umebuni na kuanzisha Mpango huu wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa PSPF. 
    Hivyo tunapenda kuzishawishi taasisi za fedha ikiwemo mabenki na wataalam wa uwekezaji na fedha kubuni njia mbalimbali za kuwasaidia wastaafu ili waweze kuwekeza na kuendelea kufurahia maisha ya ustaafu. Pia wataalam hao waangalie namna kuweka mipango ya kusaidia wastaafu hapa nchini ambao kwa ujumla wao wana kiasi kikubwa cha fedha ambacho kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchago mkubwa katika uchumi wa nchi. Mpaka sasa zaidi ya wastaafu zaidi ya 2000 wamenufaika na mpango huu ambao umeanza miezi mitatu iliyopita.
    Mstaafu anayetaka kukopa hatahitaji kuwa na dhamana , pia mkopo huu una bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake  haitaendelea kudaiwa,   aidha, riba inayotozwa kwa mkopo huu ni ndogo ukilinganisha na mikopo mingine, yaani asilimia 12 tu kwa mwaka. Wastaafu wote wa mfuko wa PSPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka moja hadi miaka mitatu.
    Ili kukopa unahitajika kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Postalililopo karibu yako


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.