May 17, 2014

  • Udanganyifu kwenye biashara ya gesi ya kupikia (LPG)

     
     
     

    Mfano wa mitungi midogo ambayo haikutimia uzito unaotakiwa.
     Salaam Ankal Michuzi.
    Tafadhali wahadharishe wadau kuhusu udanganyifu mkubwa unaofanyika hivi sasa kwenye mitungi ya gesi ya kupikia.
    Wajanja hao hupunguza gesi kutoka kwenye ile mitungi mikubwa na kupata mitungi midogo ambayo haijatimia uzito unaotakiwa.
    Jinsi ya kukwepa udanganyifu huu mkubwa ni  kuwa,  kila unaponunua gesi ya kupikia, kuhakikisha mtungi huo una "seal" kwenye sehemu ya kutolea gesi.
    Pili, usinunue mtungi wa gesi bila kuhakikisha kuwa umeupima kwenye mizani iliyopo kwa muuzaji wa gesi.
    Ni matakwa ya sheria kwamba, kila muuzaji wa gesi ya kupikia, anakuwa na mizani dukani kwake ili mteja aweze kuhakiki uzito wa mtungi anaponunua.
     
    Tafadhali mweleze rafiki,  ndugu, jamaa, jirani na hata wenzako kazini au kwenye sehemu ya biashara, ili wasikumbwe na wizi huo wa mchana.
    Tafadhali Ankal wajuze wadau wako wajihadhari, kwani taasisi husika (Wakala wa Vipimo) hata wakiwa wengi kiasi gani hawawezi kufika kila kona ya nchi hii ili wafanye kaguzi za kuwabaini Wajanja kama hao.
    Ni mimi, Mdau  wa Gesi.

     
    Jinsi gesi inavyopunguzwa toka kwenye mitungi mikubwa.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.