May 25, 2014

  • SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA KUFUNGUA SEMINA YA 24 YA CHAMA CHA MABUNGE WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA (CPA) KESHO, DAR ES SALAAM

    IMG_7500Mwenyekiti WA Sekretarieti ya Maandalizi ya Semina ya 25 ya CPA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa toka Ofisi ya Bunge, Ndg. Jossey Mwakasyuka akiongea na waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa semina hiyo. Kulia na Ndg. Elisa Mbise Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Ndg. Said Yakubu Mratibu wa CPA Kanda ya Tanzania. Picha na Owen Mwandumbya

    ………………………………………………………………………….
    Spika wa Bunge kesho tarehe 26 Mei 2014 atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina ya 25 ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola ambayo itafanyika  hapa nchini kuanzia tarehe 25/05/2014 mpaka 31/05/2014.
    Semina hiyo ambayo ni mfululizo wa hatua za mafunzo na kubadilishana uzoefu kwa Wabunge wa nchi wanachama wa CPA itahudhuriwa na Wabunge zaidi ya 60 toka nchi 18 ambazo ni Australia,  Ghana, Seychelles, Kenya Uganda na Nigeria. Nchi nyingine ni pamoja na  Sri Lanka, Bangladesh, Uingereza, NamibiaPakistan (Khyber Panktunkwa),   Kiribati , Trinidad & Tobago,  Guyana, New Zealand na Scotland. Wajumbe wengine watatoka nchi za  Zambia,  Malaysia, Swaziland, Tasmania, Cook Island,  Rajastan,  New South Wales,  Uttar Pradesh, Western Australia,   Zanzibar, Tanzania,   Chandigara, Australia Capital Territory, South Australia,    Cook Islands, na  India.
    Katika Semina hiyo, washiriki wa Semina hiyo watapata fursa ya kujadiliana mada mbalimbali ambazo ni pamoja na 
    (1)          Nafasi ya CPA katika Jumuiya ya Madola;
    (2)          Bunge na Hali ya Siasa nchini Tanzania;
    (3)          Nafasi na Jukumu la Spika na Watumishi wa Bunge;
    (4)          Mbunge na Chama cha Siasa;
    (5)          Maadili ya Bunge, Uwazi na Uwajibikaji;
    (6)          Kamati za Bunge na Mfumo wa Kamati;
    (7)          Nafasi ya Bunge katika Mapambano dhidi ya UKIMWI;
    (8)          Bunge katika kutoa haki za binadamu;
    (9)          Bunge, Mbunge na Vyombo vya Habari;
    (10)       Mahusiano ya Bunge, Serikali na Wananchi; na
    (11)       Usimamiaji wa Fedha katika Mchakato wa Kidemokrasia.
    Aidha Semina hiyo, inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mashuhuri ambao ni pamoja na 
    (1)          Mhe. Rebecca Kadaga, Mb
    Spika wa Bunge la Uganda
    (2)          Mhe. Ronald Kiandee, Mb.
    Naibu Spika wa Bunge la Malaysia,
    (3)          Mhe. Barry House
    Spika wa Jimbo la Western Australia
    (4)          Mhe. Dr. Benjamin Bewa-Nyogo Kunbour
    Mnadhimu Mkuu wa Serikali wa Ghana
    (5)          Dr. William Shija
    Katibu Mkuu wa Chama cha CPA,
    Miongoni mwa Watanzania watakaotoa mada katika Semina hiyo ni: -
    (1)          Dr. Philip Mpango
    Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango
    (2)          Dr. Ayoub Rioba
    Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
    (3)          Ndg. Ludovick Utouh
    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
    (4)          Dr. Fatma Mrisho
    Afisa Mtendaji Mkuu, TACAIDS
    Bunge la Tanzania linawakilishwa na: -
    (1)        Mhe. Job, Ndugai, Mb, Naibu Spika,
    (2)        Mhe. Mussa Zungu, Mb;
    (3)        Mhe. Beatrice Shellukindo, Mb;
    (4)        Mhe. Prof. David Mwakyusa, Mb;
    (5)        Mhe. Zahra Hamad, Mb;
    (6)        Mhe. Ummy Mwalimu, Mb;                           
    (7)        Mhe. Highness Kiwia, Mb;
    (8)        Mhe. Lediana Mng’ong’o, Mb;
    (9)        Mhe. Lucy Owenya, Mb;
    (10)     Mhe. Vita Kawawa, Mb;
    (11)     Mhe. Zaynab Vulu, Mb;
    (12)     Mhe. Khalifa Khalifa.
    Imetolewa na:
    Jossey Mwakasyuka,
    Mwenyekiti,
    Sekretarieti ya Maandalizi ya Semina ya 25 ya CPA,
    Ofisi ya Bunge,
    DAR ES SALAAM.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.