"PRESS RELEASE" TAREHE 24.05.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
MTU MMOJA BARIKO MWAKASISILE [40], MKAZI WA KIJIJI CHA NYELELE- BUJONDE WILAYA YA KYELA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS ALASIRI.
MAREHEMU ALIPIGWA JIWE KICHWANI NA LUPAKISYO JACOB, MKAZI WA KIJIJI HICHO. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.05.2014 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NYELELE, KIJIJI NA KATA YA BUJONDE TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA TUKIO HILO KINACHUNGUZWA NA MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPOKIMBILIA MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA MSAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI [02] KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA THOMAS BENEDICTO [30], MKAZI WA MBUGANI – KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 62 ZENYE UZITO WA GRAMU 460 PAMOJA NA BHANGI AMBAYO BADO HAIJASOKOTWA GRAM 500,YOTE IKIWA NA UZITO WA GRAM 960.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 08:30HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA KALUMBULU, KATA YA KYELA – KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LIMEMKAMATA MTU MMOJA MWANGOTA MWANGOTA [40], MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGU KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 70 ZENYE UZITO WA GRAMU 350.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA MBUGANI, KATA YA KYELA KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na
[ B.N.MASAKI – ACP ].
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment