Kuwa makini sana na kile unachoandika,picha unazotuma na ku-comment kwa watu kwenye mitandao ya kijamii. Mara kadhaa pasipo kufahamu nimekuwa nikikutana na watu wananiita jina kisha wanasema "huwa nasomaga sana posts zako sema huwa si-comment.
Unachokiandika na Picha unazotuma zinakusema sana wewe nii mtu wa namna gani. Unachokiandika hapa hujui kinakwenda mpaka wapi wenzako tumewahi kuitwa sehemu sehemu kutoa maelezo ya ziada. Kuna waajiri kadhaa ambao hupita kwenye mitandao unashangaa haupati kazi kumbe unayoyafanya kwenye mitandao ndizo zinazokukosesha.
Kuna watu wamewahi kupata kazi nzuri na fursa kadhaa kwa sababu vitu wanavyoviongea kwenye mitandao. Kuna watu wamekuwa wakitongozwa hovyo kwa sababu wanaume wanadhani wewe ni Malaya kutokana na picha zako.
Niliwahi sema kila unachoposti kwenye public utakuwa accountable nacho.
Kuna watu wamewahi pata wapenzi wa kweli kupitia mitandao wapo waliowahi tapeliwa, bakwa hata kufedheheshwa sababu ya muonekano.
Kama unadhani only kama unadhani kuwa unahitaji kuheshimiwa basi jiheshimu.
Sio lazima wote tuandike siasa, mapenzi, mahusia, mahubiri la hasha ila unachopost jua kuwa linabeba jibu la we we ni nani.
Sio lazima wote tuandike siasa, mapenzi, mahusia, mahubiri la hasha ila unachopost jua kuwa linabeba jibu la we we ni nani.
0 comments:
Post a Comment