May 22, 2014

  • Afya:MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME-3

     
     
     


    WIKI iliyopita niliishia kwenye maelezo kuwa secondary dysmenorhea huwakumba akina mama ambao tayari wameshajifungua mtoto mmoja au zaidi lakini wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi jambo ambalo hawakuwa nalo siku za nyuma.
    Wiki hii namalizia kwa kusema kuwa hali hii huchangiwa na mambo mengi ikiwemo tatizo la kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba unaoitwa mayoma au fibroid, kuvimba kwa mji wa mimba pamoja na mirija ya uzazi, tatizo ambalo huitwa P.I.D yaani pelvic inflamatory desease.
    Mwanamke ambaye amekwisha kujifungua na ana tatizo la maumivu chini ya kitovu na wakati huohuo anatokwa na uchafu kama maziwa ya mtindi ukeni na kupata hedhi nzito ambayo ina mabonge mabonge ni vizuri akafanya uamuzi wa kumuona daktari mapema.
    Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?
    Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume, hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa umesonga kuelekea miaka 50 au zaidi.
    Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo.
    Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalam hujulikana kwa jina la hernia ambapo waswahili tunaita ngiri.
    Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu yakiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume, ambazo zinaweza kuzalishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vya mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
    Hitimisho
    Vipimo na tiba vinahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.