May 11, 2014

  • Hadi Mchungaji naye akainua mikono Juu

    MCHUNGAJI alikuwa anawaombea waumini wake akauliza;
    MCHUNGAJI: Wangapi wanataka kuokoka inueni mikono niwaombee.....hakuna aliyeinua mkono. Pedeshe mmoja akapita mbele na kupanda madhabauni na kutangaza
    PEDESHE: Jamani mchungaji anasema wanaotaka kuokoka wanyanyue mikono juu jamani.....mtoto mmoja peke yake akanyanyua mkono, pedeshe akatoa laki tatu mfukoni akampa yule mtoto.
    PEDESHE: Haya jamani ninaomba nirudie tena niwaombe wanaotaka kuokoka wanyooshe mikono juu ili Mchungaji atuombee.....watu wote wakanyanyua mikono juu, Pedeshe akamgeukia Mchungaji ili awaombee akakuta na mchungaji nae kanyanyua mkono juu.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.