Diego Costa akiwa mjini Belgrade kwa lengo la kuonana na mganga wa kienyeji.
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade nchini Serbia kumuona `Mganga wa miujiza`, Marijana Kovacevic ili amtibu na kurejea uwanjani haraka kwa ajili mchezo mkubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Mganga huyo wa Serbia anawatibu wachezaji wenye matatizo ya misuli kwa kuwawekea placenta na Costa anataka kuichezea Atletico Madrid kwenye mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid jumamosi ya wiki hii.
Costa amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya nyama aliyopata wiki iliyopita kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu nchini Hispania, La Liga dhidi ya FC Barcelona iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Atletico kufanikiwa kutwaa ubingwa. Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kuonana na mganga wa miujiza, Marijana Kovacevic
Costa (katikati) yuko hatarini kukosa mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid.
Majeruhi aliyonayo Costa kwa sasa siku zote humfanya mchezaji akae nje ya uwanja kwa siku 15 na kama hatapata nafuu, basi atakosa mechi ya Lisbon.
Kovacevic aliwahi kuwatibu wachezaji wengi wa ligi kuu akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Asernal Robin van Persie na kiungo wa Chelsea, Frank Lampard.
0 comments:
Post a Comment