Mjumbe wa Bunge Maalum                la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa                vinavyounda TCD, Mhe. John Cheyo. 
        Na Benedict Liwenga,                MAELEZO-Dodoma.
        MJUMBE wa Bunge Maalum                la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John Cheyo                amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato                mzima wa kusaka Katiba Mpya.
        Kauli hiyo imetolewa leo                na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika                kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni                ya Shirika la Habari Tanzania (TBC).
        Mhe. Cheyo amesema kuwa                ni vema viongozi kuacha kusema uongo na kuwa waungwana                katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema                kuitakia Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa                Katiba uendelee kwa amani.
        Ameongeza kuwa Taifa la                Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani                haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani                iliyopo nchini ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya                watu wasiokuwa na nia njema na nchi.
        Mhe. Cheyo ameshangazwa                kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya                kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala                hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe                wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo                sio halali.
        "Nawashangaa UKAWA kwa                kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la                Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya kutoka ndani                ya bunge hili tena kwa nguvu", alisema Mhe. Cheyo.
        Aidha, Mhe. Cheyo                amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka                kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye uwongo                huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana nia njema                ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye kumfaa kila                Mtanzania.
        "Vijana achene kuvunjika                miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani huku                mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na mchakato huu wa                Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya kazi kwa bidiii na sio                kusikiliza uwongo", alisema Mhe. Cheyo.
          
              
        Akizungumzia kuhusu TCD,                Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano                kwa ajili ya maridhiano na mapatano pale panapokuwa na                tofauti kati ya vyama vya siasa.
        "TCD ni Jukwaa kwa ajili                ya kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni meza ya                maridhiano na nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni                kuchepuka, rudini ndani kwenye njia kuu", alisisitiza Mhe.                Cheyo.
        Naye mjumbe wa Kamati                namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven Wasira                amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu wanaosema kuwa                Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu                wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha Umma wa                Tanzania.
        "Kuna watu wanasema kuwa                Bunge Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo muhimu                yanayohusu wananchi huo ni uwongo, ni mambo gani hayo                yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo mengi yameongezwa na                kuboreshwa katika mapendekezo kwa ajili ya makundi                mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu", alisema Mhe. Wasira.
        Mhe. Wasira ameongeza                kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba na                sio ibara za CCM, amewataka Watanzania nchini wafanya                uchunguzi na kusikiliza kwa kuchambua ili kupata ukweli wa                hayo.
        "Sisi tuko tayari                kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote                waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke                kudanganywa", alisema Mhe. Wasira.
        .jpg)
0 comments:
Post a Comment