Kauli                hiyo imetolewa na naibu waziri wa uchukuzi dkt Chalres                Tibeza wakati akifungua mkutano wa wakuu wa mashirika ya                hali ya hewa wa nchi wanachama wa SADC unaofanyika jijini                hapa huku akiwataka kuhakikisha viwango vya utabiri kwa                nchi hizo vinakuwa ilikuendana na changamoto zilizopo.
          Tibeza                alisema kuwa Taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa                maendeleo ya kiuchumi kwani zinasaidia kujua kesho itakuwa                na hali gani ya hewa vile vile inamsaidia hata                mkulima,mvuvi na wote kwani inasaidia kwenye maeneo mengi                hata wasafiri wanaoenda kwenye biashara zao wakisafiri kwa                kutumia ndege pia zinawasaidia hivyo ni wajibu kwa kila                mwananchi kuzifuatilia na si kuzibeza.
          Alisema                kuwa kwa sasa utabiri wa hali ya hewa hapa nchini umefikia                kiwango cha Asilimia 85% na wakahakikisha kuwa maeneo                mengi yanakuwa na vifaa vya kuwawezesha kutoa utabiri kwa                asilimia mia utakaosaidia kukua kwa sekta hiyo muhimu kwa                maendeleo ya taifa.
          Nae                Mkurugenzi wa miundombinu na huduma wa jumuiya hiyo(SADC)                Remmy Makumbe alisema kuwa nchi hizo zinachangamoto kubwa                ya kukabiliana nao ikiwemo uhaba wa vifaa utakaosaidia                kukuwa kwa viwango vya kimataifa ya utabiri wa hali ya                hewa,na kubadilishana uzoefo ikiwemo mbinu mpya za                kukabiliana na chngamoto zinazozikabili nchi wananchama.
          Alisema                kuwa pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili                jumuiya hiyo ikiwemo michongo kutotolewa kwa wakati nan                chi wanachama pia mkutano huo unajadili mapendekezo                yatakao pelekwa kwa mawaziri wan chi hizo kupitia                mapendekezo hayo.
          Aidha                kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa                TMA hapa nchi Dkt.Agnes kijazi alisema kuwa kukuwa kwa                setka hiyo ya utabiri wa hali ya hewa hapa nchini                kunatokana na kuwa na vifaa vya kisasa vinavyosaidia                utoaji wa utabiri wenye viwango na kuishauri serekali                kusaidia upatikana wa vifaa zaidi kwenye sekta hiyo.
          Dkt                Kijazi alisema kuwa mkutano huo mkuu wan chi wanachama wa                sekta ya hali ya hewa wa jumuiya ya  maendeleo ya nchi za                kusini SADC  ni mkutano wa kuratibu mapendekezo yatakayo                wasilishwa kwa mawaziri na baadae kwa wakuu wan chi                wanachama.
          Alisema                kuwa Idara hiyo inasaidia sana kisayansi kujua hali ya                hewa ikiwemo utunzaji wa mazigira ambayo yanasaidia                kutobadilika kwa hali ya hewa ya eneo Fulani la nchi hivyo                kuweza kuyaboresha mzingira yetu huku akiwataka wananchi                kutunza mazingira kwa faida ya kutobadilika kwa hali ya                hewa kwenye maeneo yao.
        
0 comments:
Post a Comment