September 17, 2014

  • WAWILI WAFARIKI, WATANO WAJERUHIWA AJALINI



    WAWILI WAFARIKI, WATANO WAJERUHIWA AJALINI
    Na John Gagarini, Kibaha

    WATU wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya magari mawili likiwemo basi dogo la abiria waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso.

    Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Athuman mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilihusisha gari aina ya Coaster likitokea kwenye msiba Musoma kwenda Jijini Dar es Salaam na kugongana na lori la mafuta.

    Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Septemba 17 mwaka huu majira ya saa 12:15 alfajiri maeneo ya Ubena Senge katika barabara ya Morogoro.

    Alisema kuwa basi hilo dogo la abiria lenye namba za usajili namba T 663 BKP lilikuwa likiendeshwa na Ally Abdul (34) lilikuwa na abiria wapatao 20 liligongana na lori hilo la mafuta aina ya Leyland  Daf lenye namba za usajili T 858 CLK na tela namba T 421 CKY mali ya kampuni ya Ramader ya Jijini Dar es Salaam lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Rashid.

    Aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Neema Mile (39) na Jane Mtani (38) ambao miili yao pamoja na majeruhi wako kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kwa ajili ya matibab u na kusubiri ndugu wa marehemu.

    Aidha alisema kuwa chanzo cha ajaili hiyo dereva wa basi hilo la abiria kuhama upande wake kutokana na uchovu na usingizi unaotokana na kuendesha gari usiku kucha bila kupumzika na inamshikilia kuhusiana na tukio hilo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.