Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh.            Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya            walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi 
                Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi 
                                 Baadhi ya            Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi            kwa Makini
                 Balozi wa            Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa            kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya 
                 Balozi wa            Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya            waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .
                Waziri              wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani              Nankumwa akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya              Ofisini kwake.
         Baadhi ya            Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya            Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa
                 Wa kwanza            Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni            akifuatilia Mkutano huo
                 Waandishi            wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho
                Francis Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni            Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na Muasisi wa Nyika Press            Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
                Kikao              kikiwa Kinaendelea 
        Waziri wa            Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi  Mh. Kondwani            Nankumwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya            pamoja na Waandishi wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya            Ofisi yake Jijini Lilongwe.
        Waziri wa              Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani              Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na              Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
        Aliyasema hayo              baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa              Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara              ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo              katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa              Nchi hizo.
        Waziri Nankhumwa              alisema  kuwa Mtoto wa Rais  wa Malawi Profesa Ather              Muthalikana  anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa              Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi              na kufanya biashara nchini Malawi hivyo hakuna sababu za              kuwepo kwa tofauti za aina  yoyote ile itayowapelekea              kuwagawa wananchi wa pande hizo.
        Aidha alisema              kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande              hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua              samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia kuwa              wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa              makabila.
        Kauli hiyo              iliungwa mkono na Balozi              wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa              hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania              na Malawi.
        Aliyasema hayo              alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya              walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi              katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili              kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za              mazingira,utalii na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana              katika nchi hizo.
        Balozi Tsere              alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani inahitajika              subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi              hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika              mahakama ya  kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi              hizo katika utatuzi wa mgogro huo.
        Hata hivyo Waandi              wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano ambayo              yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja              na mbuga za wanyama zilizopo  Malawi na Uwanja wa ndege wa              Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza              uchumi wan chi hizo.
        Katika ziara hiyo              Waandishi  wa vyombo mbalimbali walishiriki ikiwa ni pamoja              na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel              Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira na Raia Mwema.
        Vingine na              Tanzania Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka              Mwakilili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa              Ujenzi Claudio  Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
        Na Mbeya Yetu              Blog , Lilongwe Malawi.
        
0 comments:
Post a Comment