September 23, 2014

  • Picha na Video:Ujenzi wa mradi wa umeme wa mitambo inayotumia gesi asilia iliyopo kinyerezi jijini Dar-es-Salaam, umekamilika kwa asilimia 70 huku manunuzi ya mitambo hiyo kutoka nje ya nchi ikiwa nayo imewasili nchini kwa asilimia 90, jambo linalotoa matumaini ya kuwa na umeme wa uhakika nchni.



    Picha na Video:Ujenzi wa mradi wa umeme wa mitambo inayotumia gesi asilia iliyopo kinyerezi jijini Dar-es-Salaam, umekamilika kwa asilimia 70 huku manunuzi ya mitambo hiyo kutoka nje ya nchi ikiwa nayo imewasili nchini kwa asilimia 90, jambo linalotoa matumaini ya kuwa na umeme wa uhakika nchni.


     Mitambo Miwili iliyofungwa katika kituo cha KINYEREZI ONE yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220 kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183.
     Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
      Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
      Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa "Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)"  unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
      Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.

      Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mfumo wa usambazaji umeme kwenye Moja kituo cha Mradi "Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)" unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kilichopo Mbagala kitakachozalisha megawatt 100 za umeme, kituo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa huduma za umeme wa uhakika kwa wakazi wa maeneo ya Kurasini, Kigamboni, Mbagala na Maeneo ya Mkuranga kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
     Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto)  wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.