Maryam Himid/Saada                Saleh-ZJMMC 
        Waziri wa Habari                Utamaduni Utalii na Michezo,Zanzibar,Mh. Saidi Ali Mbarouk                amezitaka Taasisi zinazosimamia kupokea Watalii Kiwanja                cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume kujenga                mashirikiano ili kuondosha usumbufu kwa wageni wanaoingia                na kuotoka nchini. Ameyasema hayo alipofanya ziara                Uwanjani hapo kwa lengo la kuangalia hali halisi ya Wageni                wanaoingia na kutoka nchini.
        Waziri Mbarouk amesema                suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu                linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar kwa wageni ambao                wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao.
        Ametoa wito kwa Taasisi                husika kuhakikisha Wageni wanaoingia Zanzibar wanapata                huduma stahiki na ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote                wanapofika katika Uwanja huo wa Ndege.
        Kwa upande wake Daktari                wa kituo cha Afya uwanjani hapo Juma muhammed Juma amesema                Wanaendelea kulisimamia vyema suala la kuwakagua kwa Vifaa                maalumu Wageni wanaoingia kutoka Nchi zilizoathirika na                Ugonjwa wa Ebola.
        Amezitaja Nchi hizo kuwa                ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Liberia na                Sera lion ambapo amesema kila abiria kutoka nchi hizo                lazima Apimwe ili kuweka kinga ya Ugonjwa wa Ebola nchini.
        Hata hivyo Mkurugenzi wa                uwanja wa ndege Juma Saleh Juma ameelezea baadhi ya                changamoto zinazowakabili uwanjani hapo kuwa ni pamoja na                upungufu wa maeneo ya kukaribisha wageni,maegesho ya                Magari na Uhaba wa Wafanyakazi wanaozungumza Lunga ya                Kitaliano kutokana na Wataliano hao kutumia lugha yao tu.
        Katika ziara hiyo Waziri                Mbarouk alitembelea maeneo mbali mbali Uwanjani hapo                ikiwemo Mapokezi, Maegesho ya Ndege na Magari na sehemu ya                Mapumziko ya Abiria. 
                Waziri wa Habari                Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Saidi Ali Mbarouk                Mwenye Koti Jeupe akipewa Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa                uwanja wa ndege Juma Saleh.Katika ziara hiyo Waziri                Mbarouk alitembelea maeneo tofauti ya Uwanja wa Kimataifa                wa Abeid Aman Karume. Baadhi ya Wageni kutoka nchi tofauti                wakipata huduma kutoka Uhamiaji mara baada ya kuwasili                Uwanja wa Abeid Aman Karume. Picha na Yussuf Simai-Maelezo                Zanzibar. 
                .jpg)
.jpg)
0 comments:
Post a Comment