September 30, 2014

  • Tibaigana Aibuka na Kusema 'Wapinzani Wana Haki kuandamana'




    Tibaigana Aibuka na Kusema 'Wapinzani Wana Haki kuandamana'
    Katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu.

    "Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.

    "Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa maandamano yao," alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.

    "Nilikuwa nawaita viongozi nakaa nao tunakubaliana. Hata kama ningeambiwa na kiongozi gani nisitoe kibali, kama hakuna sababu za kweli, nilikataa kwa kuwa kisheria mimi ndiye nawajibika kama vyama vikishtaki. Ili uzuie maandamano unapaswa kuwa na sababu za msingi ambazo ukiwaeleza waandamanaji wanakuelewa."

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.