September 27, 2014

  • SERIKALI YASEMA HAKUNA MWANDISHI ALIYEPIGWA NA POLISI, WOTE NI WANACHAMA WA CHADEMA


    SERIKALI YASEMA HAKUNA MWANDISHI ALIYEPIGWA NA POLISI, WOTE NI WANACHAMA WA CHADEMA

    HUKU wadau mbalimbali wa Habari wakiendelea kulaani vikali kitendo cha Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini katika tukio lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi nchini wakati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe akijisalimisha polisi,


    Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi yoyote wa habari.


    Kauli hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini Dar Es  Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Asah Mwambene alipokuwa anatembelea miradi ya maendeleo ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mbagala Jijini Dar Es Salaam.  
    Tanesco imetimiza miaka 50 toka ianze kutoa huduma ya usambazaji nishati kwa wananchi nchini kote.
    Mmoja wa waandishi wa habari aliyekuwepo katika ziara hiyo (toka gazeti la mwananchi) alitaka kupata kauli kutoa kwa Mkurugenzi huyo kuhusiana na tukio lililofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wanahabari waliokuwepo kazini wakati Mbowe akifika Polisi.
             
    Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa Serikali alisema, hana taarifa za kupigwa kwa waandishi wa habari bali katika tukio hilo lililohusisha wanachama wa Chadema kukusanyika makao makuu ya jeshi hilo wakati kiongozi wao akijisalimisha.
        
    "Serikali haina taarifa za kupigwa kwa waandishi, nakuomba tuzungumeze vitu vingine "Alijibu Mwambene.
             
    Hata hivyo baadhi ya watu walisikika wakinong'ona wakisema; "tumemsikia mwandishi mmoja akilalamika sana kwenye vyombo vya Habari, ni Josephat Isango wa gazeti la Tanzania Daima ambaye anaeleweka kabisa kwamba ni mwanachama wa chadema." 
    Mnong'onezaji huyo alisikika akisema Isango aliwahi kugombania Ubunge kupitia chama hicho. 
    Kauli hiyo ya Mwambene inatafsiriwa tofauti na wadau wa Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali mengi kutokana na Idara ya habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja na Magazeti.
       
    Kwa Upande wake, Josephati Isango amenukuliwa akithibitisha kuwa na nia ya kumburuza mahakamani CP Chagonja, polisi watatu waliompiga pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
     
    "Nawasiliana na wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki polisi watatu, Cp Chagonja na waziri mkuu ambaye mnakumbuka alishawhi kutoa maagizo ya kupiga watu ovyo yanayotekelezwa na Polisi hivisasa,"alisema Isango.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.