September 14, 2014

  • WAKIMBIZI KAMBI YA NYARUGUSU WAMPOKEA KWA SHANGWE WAZIRI CHIKAWE WILAYANI KASULU


    WAKIMBIZI KAMBI YA NYARUGUSU WAMPOKEA KWA SHANGWE WAZIRI CHIKAWE WILAYANI KASULU
    PIX 4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwasalimia watoto wa wakimbizi wakati Waziri huyo alipokuwa anatembelea baadhi ya familia za wakimbizi hao kwa lengo la kuwasalimia pamoja na kuangalia jinsi maisha yao wanavyoyaendesha kambini hapo. Waziri Chikawe alifanya mkutano na wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani na pia kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

    1410623790147_wps_150_vlcsnap_2014_09_13_16h41mWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kambi hiyo inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Katika hotuba yake Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi hao kupinga ndoa za utoto ambazo zinaendelezwa na baadhi ya familia za wakimbizi hao ambapo inawasababishia watoto hao wa kike kupata matatizo mbalimbali wakati wanapojifungua. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
    PIX 1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiwasalimia wacheza ngoma ya asili ya nchini Kongo iliyokuwa ikichezwa na wakimbizi wenye asili hiyo wakati alipokuwa anaingia katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma kwa ajili ya kuzungumza nao. Waziri Chikawe alifanya mkutano na baadhi ya wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
    PIX 3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika kambi hiyo, aliwataka wakimbizi hao wadumishe amani pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zimeshika kasi katika kambi hiyo kubwa ambayo ina wahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kushoto kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.