Wakaguzi kutoka shirika la ugavi wa umeme nchini Tanesco mkoa wa Arusha wakiwa na askari mgambo wamefanya operesheni ya kushitukiza katika maeneo ya Arusha mjini na Ngaramtoni wilayani Arumeru na kufanikiwa kuwakamata watu thelathini wanaodaiwa kujiunganishia umeme kienyeji ambao baadhi yao pamoja na kuwekwa chini ya ulinzi wamefanikiwa kutoroka.
Ukaguzi huo ulianza kwa mabishano kati ya wakaguzi na baadhi ya wateja wanaodaiwa kukiuka taratibu ambao wanahisi kuwa wameonewa na kulalamika kutotendewa haki.
Katika hali isiyo ya kawaida wakaguzi hao walilazimika kuvunja sehemu ya stoo katika baadhi ya nyumba hili kuwapata watu waliyojificha baada ya kuona askari na wakaguzi hao na walipopatikana akiwemo bwana Ismail Gidion aliyekutwa na kosa la kujiunganishia umeme kinyeji amejitetea kuwa yeye atambui kinachoendelea hata hivyo alifanikiwa kutoroka na kuwa kimbia wakaguzi wa shirika hilo ambo walimkimbiza bila mafanikio.
0 comments:
Post a Comment