September 12, 2014

  • Mashindano ya Safari Pool Taifa yafunguliwa rasmi mjini Moshi,Kilimanjaro leo



    Mashindano ya Safari Pool Taifa yafunguliwa rasmi mjini Moshi,Kilimanjaro leo
    Katiba Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini,Remida Ibrahim(wa pili kulia) akicheza kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Pool Taifa yajulikanayo kama "Safari National Pool Competition 2014" yanayofanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mkoani Kilimanjaro.Kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga,Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
    Baadhi ya Wachezaji wa Pool wakiwa na zawadi mbalimbali wakielekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kutoa kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama "Safari National Pool Competition 2014".
    Baadhi ya wachezaji wa Pool wakitoa zawadi za vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama "Safari National Pool Competition 2014".


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.