Kamanda                    wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP AHMED Z. MSANGI                        (pichani) anawatangazia Wananchi wote ya                    kuwa vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na                    cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa                    kujiunga na Jeshi la Polisi, Usaili huo utafanyika                    kuanzia Tarehe 28.09.2014 hadi Tarehe                        01.10.2014kuanzia majira ya saa 08:00                        Asubuhi hadi saa 16:00 jionikatika                    Shule ya Sekondari Mbeya Day.                                                   Muhimu:                 ·                            Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake                    vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results                    slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi                    ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate).                    Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.                 ·                            Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha                    endapo atachaguliwa.                 ·                            Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia                    usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la                    usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili                    ya usaili wa kuandika.                  Ni                      muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia tarehe ya                      usaili na muda wa kuanza usaili.                                                                                                                        |             
0 comments:
Post a Comment